Tahadhari ya kiafya kwa watumiaji wa tarumbeta na ala nyingine za muziki

Tatumbeta Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Madaktari wanawashauri wanamuziki kuzingatia usafi wa hali ya juu.

Wanamuziki wanaotumia vifaa vya hewa kama vile Tarumbeta na zumari, muwe makini kwani vinaweza kuwasababishia madhara ya kiafya, madaktari wa Uingereza wameonya katika jarida la Thorax.

Walielezea kisa cha ugonjwa wa nadra lakini unaoweza kuua ambao kwa sasa wanauita "bagpipe lung" katika mgonjwa wa miaka 61.

Mwanamume huyo anadhaniwa kuwa alipata uvimbe na vimelea (kuvu) vilivyoota kwenye sehemu ya ndani ya mfumo wa hewa.

Madaktari wanawashauri wanamuziki kuzingatia usafi wa hali ya juu.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Mgonjwa alipatikana na uvimbe na vimelea (kuvu kwenye sehemu yake ya ndani ya mfumo wa hewa

Wanasema kuwa vifaa vya muziki vinapaswa kusafishwa mara kwa mara kuzuia mkusanyiko wa bakteria na vimelea vingine hatari.

Na mchezaji yeyote wa vifaa hivyo ambae atapata matatizo ya kupumua na kuanza kukohowa hana budi kufikiria juu uwezekano wa dalili hizo kusababishwa na matumizi ya zana za muziki anazotumia.

Kumekuwa na taarifa nyingine sawia kuhusu matatizo ya mapafu kuhusiana na matumizi ya zumari na tarumbeta zinazochezwa katika muziki.