Rais wa Zambia atakiwa kusubiri kwa muda mrefu kuapishwa

Edger Lungu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption katiba ya Zambia inasema sherehe zozote za kuapishwa kwa rais zitacheleweshwa hadi pale mahakama ya katiba itakapoamua juu ya kesi hii.

Rais mteule wa Zambia Edgar Lungu amelazimika kusubiri kwa muda mrefu zaidi kuapishwa, kufuatia Mahakama ya kikatiba kuahirisha kesi iliyosilishwa mahakamani kupinga ushindi wake hadi hapo kesho Jumatano mchana.

Mahakama itakua ikichunguza madai ya upinzani ya kutaka kura zihesabiwe upya katika uchaguzi ambao Bw Lungu alishinda kwa asilimia 50.35% ya kura.

Alipaswa kuapishwa rasmi kama rais leo, lakini katiba ya Zambia inasema sherehe zozote za kuapishwa kwa rais zitacheleweshwa hadi pale mahakama ya katiba itakapoamua juu ya kesi hii.

Kwa hiyo kuahirishwa kwa kesi hiyo kunafanya sherehe hizo hata zichelewe zaidi.