Vichocheo vya mwili mbadala (hormone) vyaweza kusababisha saratani

Saratani ya matiti
Maelezo ya picha,

Wanawake wanaotumia dozi ya vichocheo vya mwili mbadala aina ya progesterone na oestrogen kwa pamoja walibainika kuwa na uwezo zaidi wa kupata saratani ya matiti

Utafiti mpya umebaini kuwa uwezekano wa kupata saratani ya matiti kwa wanawake wanaotumia dozi mchanganyiko ya vichocheo vya mwili (hormone) mbadala haukutiliwa maanani katika tafiti zilizopita.

Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Saratani ilibainisha kuwa wanawake wanaotumia dozi ya vichocheo vya mwili mbadala aina ya progesterone na oestrogen kwa pamoja walikua na uwezekano wa karibu mara tatu wa kupata saratani kuliko wale ambao hawajawahi kutumia dawa hiyo.

Maelezo ya picha,

Kuna haja ya kuendeleza utafiti zaidi kuhusu uhusiano wa matumizi ya vichocheo vya mwili mbadala na hatari yake ya kusababisha saratani ya matiti

Hata hivyo, Taasisi hiyo iliongeza kuwa hatari na faida ya matibabu ya dawa hizo kwa mtu binafsi vilitegemea mambo mengi ikiwemo historia ya matibabu .

Ripoti hiyo iliendelea kusema kuwa hatari ya juu zaidi iliyobainiwa na utafiti wa sasa ikilinganishwa na tafiti za awali, inaonyesha haja ya kufanya utafiti zaidi kuhusu suala hili.