'Watalii wa kujitolea' wanavyotishia maendeleo Afrika

'Watalii wa kujitolea' wanavyotishia maendeleo Afrika

Utalii kupitia kujitolea, umekuwa mbinu mpya zaidi ya wageni kusafiri mataifa yanayoendelea huku idadi yao ikikadiriwa kuwa wageni milioni moja nukta sita kila mwaka.

Utalii huu unamaanisha watu kutoka mataifa ya magharibi wanasafiri nchi nyingine kwa madai kuwa wanakuja kuwasaidia watu katika jamii.

Wengi wao wanaaminiwa kwenda Afrika. Lakini sasa utalii huu umetajwa kuwa tishio zaidi kwa maendeleo ya jamii hizo badala ya kuwa faida.

Mwandishi wa BBC Nancy Kacungira anaripoti kutoka Nairobi.