Marekani yawawekea vikwazo wanawe Joseph Kony

Joseph Kony
Image caption Kiongozi wa LRA Joseph Kony anasakwa kwa uhalifu wa kivita

Marekani imesema kuwa imeweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya watoto wawili wa kiume wa kiongozi wa kundi la Lord's Resistance Army (LRA) leader Joseph, ikiwashutumu kuhusika katika biashara haramu ya kusafirisha pembe za ndovu.

Salim Kony na Ali Cony walikua makamanda wa LRA waliokuwa na '' nafasi kubwa " katika biashara ya usafirishaji wa pembe za ndovu kutoka mbuga ya wanyama ya Garamba iliyopo kaskazini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kupitia taifa jirani la Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR) hadi katika jimbo linalozozaniwa la Kafia Kingi kwa ajili ya mauzo ama biashara na wanunuzi wa jimbo hilo, ilieleza kauli ya mamlaka ya hazina ya Marekani.

Huku Salim akiratibu shughuli za usafiri wa pembe za ndovu, Ali amekua muhusika mkuu katika kujadili na wafanya biashara viwango vya bei na huuza pembe hizo kwa dola ama pauni ya Sudan, ame kwa mauzo ya ya pembe za ndovu kwa silaha , makombora, na chakula na wachuuzi wa Kafia Kingi."

Mali yoyote inayomilikiwa na wanaume hao wawili nchin Marekani nchini Marekani itafujwa na "kwa ujumla" raia wa Marekani wanazuiwa kufanya biashara nao, alisema mkuu wa hazina .

Kundi la LRA liliundwa nchini Uganda, lakini lilifurushwa nchini humo na vikosi vya serikali.

Wapiganaji wake sasa wamekua wa kuhama hama katika maeneo ya misitu mikubwa ya DRC na Jamuhuri ya Afrika ya kati.