Mafuriko yasababisha vifo kaskazini mwa India

Chanzo cha picha, AFP
Mafuriko katika jimbo la Bihar
Mafuriko makubwa yaliyokumba eneo la kaskazini na kati ya India yamesababisha vifo vya zaidi ya watu mia moja hamsini.
Kwa mujibu wa serikali watu wengine milioni mbili nukta nne wameathiriwa katika jimbo la Bihar na miji mingine ya mashariki huku viwango vya maji katika mto Ganges vikizidi kuongezeka.
Chanzo cha picha, AFP
Watu watafuta makao Bihar
Maelfu ya watu wamepewa hifadi katika kambi lakini wengine hawataki kuondoka majumbani mwao.
Shirika la misaada la ActionAid limesema kumekuwa na uharibifu mkubwa hasa katika mashamba ya mpunga ambao huenda kukasababisha upungufu wa chakula.