Sababu ya vijana wa CCM kupanga maandamano
Huwezi kusikiliza tena

Sababu ya vijana wa CCM kupanga maandamano Tanzania

Kumekuwa na maoni tofauti nchini Tanzania siku moja baada ya Umoja wa vijana wa Chama tawala CCM nchini Tanzania kutangaza maandamanona mikutano ya hadhara nchini nzima ifikapo Agosti 31 mwaka huu.

Tayari upinzani wa nchi hiyo nao wameshatangaza kufanya maandamano kama hayo ifikapo Septemba mosi mwaka huu ikiwa ni siku moja baada ya hayo ya vijana wa CCM.

Maandamano hayo yanatangazwa wakati jeshi la Polisi la nchi hiyo likiwa limepiga marufuku maandamano na mikutano ya yoyote ya kisiasa.

Mwandishi wetu Arnold Kayanda amezungumza na Shaka Hamdu Shaka Kaimu Katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa CCM na kumuuliza kwanini wameamua kufanya maandamano wakati yamezuiwa na polisi.