Donde: Wakenya wamekuwa wakihangaishwa na benki
Huwezi kusikiliza tena

Donde: Wakenya wamekuwa wakihangaishwa na benki

Rais Uhuru Keyatta ametia saini mswada uliozua mzozo wa kudhibiti viwango vya riba kwa mikopo ya benki.

Benki za kibiashara zilikuwa zimetoa wito kwa serikali kutoidhinisha mswada huo kuwa sheria licha ya shinikizo kubwa kutoka kwa upinzani na raia.

Ili kupata tathmini kamili kuhusu mzozo huu, mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amezungumza na Bw Joe donde, ambaye ni mchumi na mbunge wa zamani ambaye alianzisha juhudi za kuitaka serikali idhibiti viwango vya riba.