Wanasiasa Kenya wanawajali vijana?
Huwezi kusikiliza tena

Wanasiasa Kenya wanawajali vijana?

Nchini Kenya vyama vya kisiasa viko mbioni kwa mipangilio ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Ikiwa imesalia chini ya mwaka mmoja kabla ya kura kupigwa, mirengo mipya ya kisiasa imechipuka, vyama vipya vya kisiasa vimetangazwa na mazungumzo ya miungano inaendelea.

Hata hivyo swali linaloonekana kutotiliwa maanani ni je, Vyama vya kisiasa, vinajali maslahi ya vijana?

Ndiyo mada kuu ambayo vijana wanaangazia kuhusu mchango wao katika vyama vya kisiasa.