Sarkozy: Burkini inatumiwa kufanya ‘uchokozi’

Bw Nicolas Sarkozy Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bw Nicolas Sarkozy

Rais wa zamani wa Ufaransa mwenye msimamo mkali, Nicolas Sarkozy, amesema vazi la kuogelea linalofunika mwili mzima linalovaliwa na wanawake wa Kiislamu, ambalo linafahamika kama Burkini, kwamba linatumiwa kufanya "uchokozi".

Amesema linaunga mkono itikadi kali.

Visa vya kupigwa marufuku vazi hilo la kuogelea ambavyo vimekua vikiendelezwa katika miji mbali mbali nchini Ufaransa vimezua mjadala mkali katika taifa hilo .

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Bw Sarkozy alisema kwenye mahojiano ya televisheni Jumatano usiku kwamba „Hatuwafungi wanawake jela kwa vazi."

Kama kiongozi mashuhuri wa upinzani , Sarkozy alitangaza wiki hii kwamba atagombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao.

Lakini lazima kwanza ashinde kura za mchujo zitakazoandaliwa na chama cha mrengo wa kulia cha Ufaransa mwezi Novemba mwaka huu, ambako anatarajiwa kukabiliwa na ushindani mkubwa.

Sarkozy anasema ikiwa atashinda, atapiga marufuku ishara zozote za kidini kidini katika vyuo vikuu vya Ufaransa.

Katika kampeni zake Sarkozy, mwenye umri wa mika 61, anatarajiwa kusisitiza juu ya kuwekwa kwa sheria kali dhidi ya uhamiaji na masuala ya usalama wa nchi kutokana na mashambulio ya hivi karibuni yaliyotekelezwa na Waislamu wenye itikadi kali

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha TF1 channel, Sarkozy alisisitiza kwamba Waislamu nchini Ufaransa ni watu wa Ufaransa ``sawa kabisa na watu wengine'' lakini, wanapoishi katika nchi wanapaswa ``kusoma na kuiga ' 'lugha ya kifaransa na namna wafaransa wanavyoishi, mikoa ya Ufaransa na historia ya Ufaransa.

Haki miliki ya picha VANTAGENEWS
Image caption Watalii katika ufuo wa bahari kusini mwa mji wa Nice ambapo mwanamke alilazimishwa kuvua Burkini

Waislamu hawapaswi ``kulazimisha tofauti zao kwa watu walio wengi,'' alisema.

Hivi karibuni, Sarkozy alisema kuwa Ufaransa kama nchi isiyo na misingi ya kidini, inapinga kuwepo kwa utaratibu unaowekwa na baadhi ya hoteli za wanafunzi ambazo haziuzi nyama ya nguruwe kwa watoto wa Kiislamu na Wayahudi.

Pia alipendekeza kuwa watoto wanaozaliwa Ufaransa kwa wazazi wanaoishi kinyume cha sheria nchini humo hawapaswi kupewa uraia wa Ufaransa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii