Bendi ya muziki ya polisi  wa Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Polisi nchini Uganda wamezindua muziki unaopongeza kazi ya polisi

Polisi nchini Uganda wamezindua muziki ambao maudhui ya wimbo huo,yamejaa pongezi kwa maafisa wake kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Hata hivyo pamoja na kujipongeza huko, Polisi nchini Uganda imelaumiwa kwa kutumia mkono wa chuma dhidi ya raia hasa wale wa upinzani wanaotoka kambi upinzani ya chama cha FDC ya Dr Kiiza Besigye .

Mwandishi wetu wa Kampala Siraj kalyango amezungumza na Afande Miah,mmoja wa waliotunga na kuimba wimbo huo unaojuliaka kwa jina la Kazi Yetu..