Mapigano kusitishwa rasmi Jumatatu nchini Colombia

Farc walitangaza kusitisha mashambulizi mwaka mmoja uliopita
Image caption Farc walitangaza kusitisha mashambulizi mwaka mmoja uliopita

Siku mbili baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani baina ya waasi na serikali juu ya mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 50 nchini Colombia, Rais wa nchi hiyo Juan Manuel Santos ametoa amri kwa jeshi kusimamisha mapigano dhidi ya kundi la waasi la Farc.

Rais Santos amesema mapigano yatasitishwa kuanzia usiku wa jumatatu.

Farc walitangaza kusitisha mashambulizi mwaka mmoja uliopita.

Hata hivyo mbali na uamuzi wa serikali ya Colombia kusitisha mashambulizi dhidi ya waasi lakini imekataa kutoa taarifa rasmi za kijeshi mpaka makubaliano yatakapo kamilika.

Image caption Rais Santos amesema mapigano yatasitishwa kuanzia usiku wa jumatatu

Mkataba wa makubaliano ya amani bado unasubiri kupitishwa na wananchi wa Colombia kwa kura yha maoni.