Waokoaji waendeleza kasi kuokoa maisha ya watu Italia

Watu wengi bado hawajulikani walipo
Image caption Watu wengi bado hawajulikani walipo

Timu ya waokoaji katikati ya Italia inajitahidi kuendelea kuokoa maisha ya watu ambao bado wako hai kufuatia tetemeko la Ardhi lililoathiri miji mitatu na kuua watu zaidi ya 250.

Mamia ya wengine wamejeruhiwa.

Upekuzi ambao umefanywa kwa siku mbili unakwamishwa na mishindo yenye nguvu.

Image caption Uharibifu mkubwa umetokea

Mshindo mkubwa ni ule uliotokea katika mji wa Amatrice ambapo waokoaji walikimbia kutokana na kuangukiwa na uchafu.

Image caption Mtoto aliyefukuliwa kwenye kifusi akiwa hai

Serikali ya Italia imetangaza hali ya hatari kwa maeneo yaliyokubwa na tetemeko la ardhi na kutangaza kutoa euro milioni hamsini kutoka mfuko wa dharura.