Meli ya Marekani yakumbana na vikwazo katika bahari ya Iran

Amesema tabia ya Iran haikubaliki na ikizingatiwa kwamba meli ilikuwa kwenye mpaka wa maji wa kimataifa
Image caption Amesema tabia ya Iran haikubaliki na ikizingatiwa kwamba meli ilikuwa kwenye mpaka wa maji wa kimataifa

Idara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa moja ya meli zake imetupa makombora ya kuonya baada ya boti moja iendayo haraka ya Iran kuikaribia Meli ya Marekani.

Msemaji wa Pentagon Peter Cook amesema kumekuwa na matukio kadhaa ndani ya wiki hii ambapo meli za Iran zilifanya kile ambacho kinatafsiriwa kama kutokuwa na usalama na ukosefu wa taaluma.

Katika namna moja manuwari za Iran zimeripotiwa kuja karibu kwa zaidi ya mita mia mbili na meli za Marekani.

Amesema tabia ya Iran haikubaliki na ikizingatiwa kwamba meli ilikuwa kwenye mpaka wa maji wa kimataifa.

Waziri wa ulinzi wa Iran Generali Hosein Deh-ghan ametaarifu kwa kusema kuwa msako kama huo utaendelea ili kutoa changamoto kwa meli za kigeni zinazoingia kwenye maji ya Iran.