Washambuliaji waua watu saba ufukweni Somalia

Washambuliaji wawili waliuawa na mmoja akakamatwa, polisi wa Somalia wamesema Haki miliki ya picha EPA
Image caption Washambuliaji wawili waliuawa na mmoja akakamatwa, polisi wa Somalia wamesema

Watu wenye silaha wameshambulia mgahawa mmoja wa ufukweni mjini Mogadishu na kuwaua watu saba.

Shambulio lilianza kwa mlipuko wa bomu la kutegwa kwenye gari nje kidogo ya mgahawa wa Beach Club in eneo la Lido.

Baadaye, kulitokea ufyatulianaji mkali wa risasi.

Polisi wanasema washambuliaji wawili waliuawa wakati wa shambulio hilo lililotekelewa Alhamisi jioni.

Mshambuliaji wa tatu amejeruhiwa na anakamatwa.

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al Shabaab hutekeleza mashambulio ya moja kwa moja Mogadishu na maeneo mengine ya Somalia.

Mapema mwaka huu, watu 17 walifariki baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kushambulia mgahawa mwingine katika ufukwe wa Lido.