Diamond: Usitosheke kuvuma nyumbani pekee
Huwezi kusikiliza tena

Diamond Platinumz: Usitosheke kuvuma nyumbani pekee

Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu kama Diamond ni mmoja kati ya wanamuziki maarufu nchini Tanzania na Afrika mashariki, lakini pia mwanamuziki aliyejizolea tuzo za ubora.

Hivi karibuni ameibuka na kibao chake kipya kinachoitwa Kidogo akishirikiana na P Square.

Wimbo wake huo kwa sasa umevuka mipaka na kuingia hadi katika chati za BBC London, kipindi cha BBC One Extra playlist, kinachosheheni tungo bora kutoka duniani kote.

Mwandishi wa BBC David Nkya alimtembela Diamond Platnum na kuandaa taarifa ifuatayo.