Utata kuhusu marufuku ya mikutano ya kisiasa Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Utata kuhusu marufuku ya mikutano ya kisiasa Tanzania

Kumekuwa na maoni tofauti nchini Tanzania baada ya Polisi Nchini humo kupiga marufuku mikutano yote ya ndani ya kisiasa katika hatua ambayo wadadisi wanasema ni jaribio la kukandamiza demkrasia.

Tangazo hilo linafuatia mauaji ya maafisa wanne wa polisi siku ya jumanne katika mji mkuu wa Dar es Salam, mauaji ambayo Polisi inadai yalichochewa kisiasa.

Tayari maandamano na mikutano yote ya hadhara ya kisiasa imeshapigwa marufuku na polisi nchini Tanzania.

"Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, kimeshutumu hatua hiyo."

Kutoka Dar es Salaam Mwandishi wetu Ester Namuhisa ametuandalia taarifa ifuatayo.