Kwa Picha: Afrika Wiki Hii: 19-25 Agosti 2016

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za matukio muhimu barani Afrika, na picha za Waafrika kutoka maeneo mengine ulimwenguni, wiki hii.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msanii asimama mbele ya bidhaa zake za sanaa katika tamasha la mtaa wa Chale Wote, Acrra Ghana, siku ya Jumapili.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakati wa kujipodoa...! Katika tamasha la sanaa kwenye mkoa wa kihistoria wa James Town mjini Accra.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption ... Wakati wa kutumbuiza umati kwa miondoko ya aina yake!
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku mbili baadaye, wapiga zumari wa kitamaduni wamtumbuiza waziri wa maswala ya nje wa Marekani John Kerry kwenye makao makuu ya mtawala wa Sokoto, kiongozi wa kiislamu mwenye ushawishi mkubwa, Nigeria.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wakenya wamwandikia bwana Kerry ujumbe kwenye hoteli moja mjini Nairobi, ambapo alikutana na viongozi wa kisiasa wa kikanda, siku moja kabla ya kushiriki mazungumzo ya amani Sudan Kusini na Somalia.
Haki miliki ya picha AP
Image caption Ijumaa, jua laonekana likitua juu ya piramidi na mto Nile, katika mji mkuu wa Misri, Cairo.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Karibu na eneo hilo, fundi afanya marekebisho ya mabaki ya kaburi la mfalme Tutankhamun siku ya Jumapili, kwenye makavazi ya Grand Egyptian Museum, jengo kubwa linatarajiwa kufunguliwa baada ya miaka michache ijayo.
Haki miliki ya picha AP
Image caption Fahari kwa wanawake wa Kiafrika! Washindi wa mbio za mita 800 katika michezo ya olimpiki mjini Rio: Francine Niyonsaba wa Burundi, Caster Semenya wa Afrika Kusini na Mkenya Margaret Wambui.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumanne, 23 Agosti 2016, Gabon: Mwanamme avalia kofia ya manyoya wakati wa mkutano wa kisiasa kabla ya uchaguzi wa urais ambapo rais Ali Bongo anakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa aliyekuwa kamishna mkuu wa Umoja wa Afrika Jean Ping.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Siku iyo hiyo, mkulima wa tumbaku apumzika karibu na vifungu vya tumbaku sokoni mjini Harrare nchini Zimbabwe.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwendesha pikipiki aonyesha ueledi wake siku ya Jumanne mjini Nairobi, wakati wa mashindano ya pipiki ya ubingwa wa bara Afrika