Wakuu wa makanisa ya Kikristo wamemshutumu John Kerry kwa kuwabagua wakristo

John Kerry na Sultan wa Sokoto Haki miliki ya picha AFP
Image caption John Kerry alikutana na Sultani wa Sokoto, Kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa kiislam nchini Nigeria Jumanne

Madhehebu makuu ya kikristo nchini Nigeria yamemshtutumu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kwa kuchochea mgawanyiko wa kidini wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini humo.

John Kerry alifanya kitendo cha ubaguzi cha mgawanyo kwa na ubaguzi kwa kuzulu eneo la kaskazini mwa Nigeria linalokaliwa na Waislam , na kukutana na sultani wa Sokoto na viongozi wengine wa kaskazi, imeeleza Jumuiya ya Wakristo Nchini Nigeria (Can).

Ukusefu wake wa "heshima kwa watu wa tabaka mbali mbali nchini Nigeria, kumemfanya kuwapendelea watu wa kaskazini mwa Nigeria na waislam kwa kuimiza jumuiya ya wakristo ", gazeti la Premium Times limemnukuu Supo Ayokunle, rais wa Can akisema .

Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Marekani hadi sasa kuhusiana na kauli hizo.

Ziara ya hivi karibuni ya Bw Kerry katika nchi za Kenya na nigeria wiki hii iliangazia juu ya masula ya usalama.

Eneo la kaskazini mwa Nigeria limeathiriwa na uasi wa kundi la kiislam la Boko Haram katika kipindi cha miaka saba iliyopita.