Kongamano la Japan Nairobi litafaa Afrika?
Huwezi kusikiliza tena

Kongamano la Japan Nairobi litafaa Afrika?

Kongamano hili limefanyika Afrika kwa mara ya kwanza na lengo la kuhakikisha nchi za afrika kwamba zinamiliki mchakato wa TICAD.

Kwa sasa Afrika kusini ndio mshiriki mkuu wa kibiashara wa japan barani afrika. Japan yenyewe ambayo ishakilia nafasi ya pili katika uchumi duniani, ndio mfadhili nambari nane katika mataifa ya afrika ikiwa imewekeza zaidi ya dola za marekani billioni moja.

Wakati huu ambao Japan imeanza kujihusisha zaidi na mataifa ya afrika, wachambuzi wanasema kwamba ni njia ya kupambana na ushawishi wa China katika bara afrika.

Mwanahabari wa BBC Paula Odek, amezungumza na katibu mkuu wizara ya mambo ya nje nchini Kenya, Monica Juma ambaye anafafanua kwa kina kuhusu yanayotarajiwa kufikiwa katika kongamano hilo.