Polisi wakabiliana na waandamanaji wa Upinzani Zimbabwe

Haki miliki ya picha AP
Image caption Makabiliano yalichacha pale waandamanaji walipoamua kujibu mashambulio ya polisi kwa kuwarushia mawe na kuchoma mataili ya gari

Polisi wamefyatua gesi za kutolea machozi na mabomba ya maji katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare, kinyume na amri iliyotolewa na mahakama iliyowataka kutoingilia kati maandamano.

Makabiliano yalichacha pale waandamanaji walipoamua kujibu mashambulio ya polisi kwa kuwarushia mawe na kuchoma mataili ya magari.

Kiongozi wa upinzani Joice Mujuru amesema kuwa zaidi ya watu hamsini wamejeruhiwa.

Makundi ya upinzani yaliandaa maandamani kushinikiza mageuzi ya sheria ya uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwandamanaji akionyesha bango lililong'olewa kwenye barabara ya Robert Mugabe wakati wa maandamano ya kupinga serikali

Robert Mugabe --mwenye umri wa miaka 92 anasema anatarajia kugombea kiti hicho.

Kumekuwa na ongezeko la idadi ya maandamano ya upinzani dhidi ya serikali nchini Zimbabwe.