Australia: Kijana mwenye miaka 18 amudu kuendesha ndege ya injini moja

Haki miliki ya picha ABC
Image caption Bw Smart alitumia muda wa takriban miezi miwili kukamilisha safari yake, ambapo aliweza kutua katika viwanja ishirini na vinne.

Kijana mdogo raia wa Australia amekuwa wa kwanza mtu mdogo zaidi kwa umri kote duniani kuendesha ndege yenye injini moja.

Akiwa na umri wa miaka kumi na minane tu , Lachlan Smart ni mdogo kwa mwaka mmoja chini ya raia wa Marekani iliyekua akishikilia rekodi hiyo.

Bw Smart alitumia muda wa takriban miezi miwili kukamilisha safari yake, ambapo aliweza kutua katika viwanja ishirini na vinne.

baada ya kurejea kwenye uwanja wa ndege wa Queensland ambako alianzia safari yake , kijana huyo alisema anachotamani ni kulala kwenye kitanda chake tena.