Daktari wa Trump akiri kuandika waraka uliosifu afya yake

Donald Trump Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Barua ya Dr Bornstein ilisema Bw Trump, mwenye umri wa miaka 70, atakuwa "ndiye mtu binafsi mwenye afya aliyewahi kuchaguliwa kuwa rais".

Daktari wa Donald Trump' amesema alitumia dakika tano kuandika barua kuidhinisha afya ya mgombea wa urais wa chama cha Republican,huku gari la Bw Trump likimsubiri nje.

" kwa haraka nadhani baadhi ya maneno hayo hayakueleza bayana kile yalicho maanisha ," Dr Harold Bornstein alikieleza kituo cha habari cha NBC.

Barua ya Dr Bornstein ilisema Bw Trump, mwenye umri wa miaka 70, atakuwa "ndiye mtu binafsi mwenye afya aliyewahi kuchaguliwa kuwa rais".

Alisema "alitumia "lugha ya ukarimu" alipokuwa akiandika waraka huo.

Wiki mbili kabla ya kuandikwa kwa waraka huo, Bw Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter kwamba "nilimuagiza daktari wangu wa muda mrefu kutoa, ripoti kamili ya afya yangu katika kipindi cha wiki mbili", akiongeza kuwa itaonesha "usahihi".

Baadae Bw Trump alionyesha waraka ulioidhinishwa na Dr Bornstein, ambaye alikabiliwa na maswali kuhusu lugha ya mvuto aliyoitumia kwenye waraka huo.

Daktari huyo wa hospitali ya New york ya Lenox Hill, anasema huwenda alitumia maneno ya kuvutia zaidi '' ili kuwafurahisha watu wa kampeni ya Donald trump".

"nadhani nilitumia lugha yake ya ukaribu halafu nikaibadilisha katika lugha yangu binafsi ,"alisema.

Bw Trump atakuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani, ikiwa atashinda uchaguzi wa mwezi Novemba.

Bi Clinton ana umri wa miaka 68.

Afya za wagombea hao wawili limekuwa ni suala linaloangaziwa katika kampeni, huku Bw Trump akirejerea madai kwamba hasimu wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton hana afya nzuri.

Bi Clinton alijibu kile alichosema kuwa ni madai yasiyo na msingi, na Bw Trump amekabiliwa na ukosoaji kuhusu namna anavyomshambulia Bi Clinton kuhusu suala hilo