WhatsApp kugawana data na Facebook

WhatsApp na facebook
Image caption WhatsApp na facebook

Kamishna wa mawasiliano nchini Uingereza anachunguza uamuzi wa programu ya WhatsApp wa kugawana data na kampuni ya facebook.

Data hiyo ya watumiaji wa WhatsApp itatumiwa kuvutia matangazo yanayoonekana na watumiaji wa mtandao wa facebook.

Itagawana nambari za simu na maelezo ya mara ya mwisho mteja kuingia katika akaunti yake ya WhatsApp na facebook.

Kamishna huyo amesema kuwa kwa kuwa mabadiliko hayo yataathiri watu wengi ,anataka maelezo zaidi kuhusu kile kitakachogawanywa kati ya huduma hizo mbili.

Kamishna Elizabeth Denham amesema kuwa watumiaji watakuwa na maoni tofauti kuhusu mabadiliko hayo.