Iraq yaitaka Saudia kumuondoa balozi wake

Thamer al-Sabhan Haki miliki ya picha AFP
Image caption Thamer al-Sabhan

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Iraq, imeiomba Saudi Arabia imuondoe balozi wake mjini Baghdad.

Wanasiasa wa Ki-Shia wamesema mara kadha, kwamba bwana Thamer al-Sabhan aondoshwe, baada ya matamshi ya balozi huyo, juu ya kuhusika kwa Iran nchini Iraq, akidai kuwa wanamgambo wa Ki -Shia, wanazidisha mvutano na Sunni.

Juma lilopita, wakuu wa Iraq walikanusha ripoti za vyombo vya habari, kwamba kuna njama ya kumuuwa balozi huyo.