Aliyetuhumiwa na kashfa ya kuuza tiketi Rio aachiliwa huru

Mshukiwa wa kashfa ya uuzaji tiketi katika michezo ya Olimpiki ya Rio Kevin Mallon Haki miliki ya picha AP
Image caption Mshukiwa wa kashfa ya uuzaji tiketi katika michezo ya Olimpiki ya Rio Kevin Mallon

Wakuu wa Brazil wamemtoa gerezani mfanyibiashara wa Ireland, aliyeshukiwa kuhusika na kashfa kuhusu uuzaji wa tikiti za Michezo ya Olimpiki iliyofanywa Rio.

Kevin Mallon, mkurugenzi wa kampuni moja ya takrima ya Uingereza, THG, alizuiliwa kwa siku tatu kwenye gereza lenye ulinzi mkali mjini Rio.

Alikamatwa akiwa na mamia ya tikiti, zilizokusudiwa Halmashauri ya Olimpiki ya Ireland ambapo baadhi ya tikiti zilikuwa za sherehe za ufunguzi na ufungaji wa michezo hiyo.

Kampuni ya THG imekanusha kuwa ilifanya kosa.

Wakili wa bwana Mallon, alisema kufunguliwa kwa mteja wake, hakuathiri kesi ya mtu mwengine aliyeko kizuizini kwa sababu ya kashfa kuhusu tikiti, Patrick Hickey ambaye ni mkuu wa halmashauri ya Olimpiki ya Ireland.

Mada zinazohusiana