Waasi wa Houthi wakubali mazungumzo ya amani Yemen

Waasi wa Houthi nchini Yemen Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Waasi wa Houthi nchini Yemen

Waasi wa Houthi nchini Yemen wamesema kwamba wako tayari kuanza upya mazungumzo ya amani na serikali iliyo uhamishoni ikiwa operesheni za jeshi la Saudi Arabia na washirika wake zitasitishwa.

Aidha wapiganaji hao wametaka maeneo wanayodhibiti kuachwa kuzingirwa.

Hii inafuatia tangazo la waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kwamba mpango wa kuanza mazungumzo umeafikiwa na mataifa ya ghuba na Umoja wa Mataifa.

Mpango wa sasa umewapa wapiganaji wa Houthi nafasi ya kujumuishwa kwenye serikali ya muungano ikiwa wataondoka katika mji mkuu Sanaa pamoja na kusalimisha silaha.

Mazungumzo ya awali yaliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa yaligonga mwamba kufuatia kukiukwa kwa mpango wa amani.

Waasi wa Houthi walichukua mji mkuu wa Sanaa na kutimua serikali inayotambuliwa kimataifa ya Rais Abdrabbu Mansour Hadi.

Mada zinazohusiana