Beyonce atawala tuzo za MTV Marekani

Beyonce Knowles katika tuzo za MTV
Image caption Beyonce Knowles katika tuzo za MTV

Mwanamuziki wa Marekani Beyonce alitawala tuzo za muziki za MTV mjini New York siku ya Jumapili akijipatia mataji saba.

Msanii huyo alijishindia tuzo kubwa katika tamasha hilo kwa kujishindia video ya mwaka kwa nyimbo yake 'Formation' ambayo inataja ubaguzi wa rangi,utumiaji wa nguvi kupitia kiasi unaofanywa na maafisa wa polisi pamoja na kimbunga Katrina.

Beyonce aliwasili katika tamasha hiyo na mama zao wanaume wanne Wamarekani weusi ambao vifo vyao vilizua hisia kali.

Image caption Rihanna katika tuzo za MTV

Msanii wa pili aliyeteuliwa katika tuzo hizo Adele hakujishindia kitu.

Msanii Rihanna alitunukiwa tuzo ya mchango wake katika usanii kufikia sasa akiwa na umri wa miaka 28 pekee.

Mada zinazohusiana