Shambulio la IS lawaua watu 60 Yemen

Shambulio la Islamic State nchini Yemen lawaua watu wengi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shambulio la Islamic State nchini Yemen lawaua watu wengi

Takriban watu 60 wamauawa katika shambulio la bomu la kujitolea muhanga lililolenga kambi ya mafunzo ya kijeshi eneo la Aden nchini Yemen.

Maafisa wa usalama wanasema mshambuliaji aliendesha gari lililokuwa limetegwa mabomu karibu na makurutu wapya waliokua kambini kaskazini mwa nchi.

Taarifa kutoka kwa shirika la misaada la MSF linasema maiti kadhaa zimesafirishwa katika hospitali za karibu.

Kundi la Ilsmic state limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Shambulio hilo linajiri huku kukiwa na msukumo mpya wa kusitisha vita vya miezi 17 nchini Yemeni kati ya serikali inayoungwa mkono na Saudia dhidi ya waasi wa Houthi ambapo Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban watu 6,600 wamefariki huku wakaazi milioni 2.5 wakiachwa bila makao.