Uber yasitisha huduma zake Abu Dhabi

Huduma ya texi ya Uber Haki miliki ya picha EPA
Image caption Huduma ya texi ya Uber

Kampuni ya huduma ya texi Uber imesimamisha huduma zake huko Abu Dhabi ,mji mkuu wa Umoja wa falme za Kiarabu UAE.

Huduma pinzani ya texi nchini humo Careem pia imesitisha kwa mda huduma zake baada ya baadhi ya magari yake kusimamishwa na mamlaka.

Uber ambayo imekuwa ikifanya operesheni zake katika Umoja huo wa mataifa ya kiarabu tangu mwaka 2013 haikuelezea kwa nini ilisitisha huduma zake ,lakini ikasema kuwa hatua hiyo ni ya muda.

Gazeti moja la UAE ,the National,limeripoti kwamba zaidi ya madereva 50 walikamatwa wikendi iliopita.

Ripoti hiyo imemnukuu mtu mmoja akisema kuwa haijulikani ni kwa nini madereva hao wanazuiliwa.

Hatahivyo kampuni zote mbili zimesema kuwa huduma zao zinaendelea kama kawaida katika mji wa Dubai

Mada zinazohusiana