Mwanariadha wa 2 wa Ethiopia aonyesha ishara ya kupinga serikali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ishara ya "x" hutumiwa kupinga nchini Ehiopia

Juma moja baada mwanariadha wa Ethiopia Feyisa Lilesa, ambaye alishinda fedha katika mashindano yaliyokamilika ya mjini Rio kugonga vyombo vya habari baada ya kufanya ishara ya kupinga akitumia miakono yake alipokuwa akikamilisha mbio hizo, sasa mwanariadha mwingine wa Ethiopia amekamilisha mbio za Quebec kwa kufanya ishara kama hiyo.

Ishara hiyo hufanywa na watu wa kabila la Oromo nchini Ethiopia, ambao wametaabika kutokana na dhuluma zinazofanywa na polisi.

Mtandaoa wa twitter nchini Canada uliandika habari wakati Ebisa Ejigu, alishinda mbio kwa muda wa 2:30:40 na kufanya ishara hiyo ya kupinga kwa mikono.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eneo la Oromia ndilo kubwa zaidi nchini Ethiopia na limekumbwa na maandamano kwa kipindi cha miezi 26 iliyopita.

Baada ya kufanya ishara hiyo mjini Rio, Feyisa hajarejea nchini Ethiopia akisema kuwa anahofia maisha yake au anaweza kufungwa jela.

Shirika la kupigania haki za binadamu la Amnesty International, linasema kuwa watu 97 waliuawa wakati vikosi vya usalama vilifyatua risasi kwenda kwa maandamano ya amani.

Feyisa alizaliwa eneo la Ambo huko Oromia ambalo ndilo kubwa zaidi nchini Ethiopia na ambalo limekumbwa na maandamano kwa kipindi cha miezi 26 iliyopita.