Wanafunzi weusi wapinga amri ya kuwataka walainishe nywele

Image caption Wanafunzi wanasema kuwa amri hiyo ni ya kibaguzi

Kumeshuhudiwa maandamano kwenye shule moja ya wasichana nchini Afrika Kusini baada ya wanafunzi weusi kuambiwa na shule moja mjini Pretoria, wazilainishe nywele zao.

Mwandishi wa BBC mjini Pretoria anasema kuwa wanafunzi wamekusanyika katika shule moja mjini humo baadhi ya wakibeba mabango.

Image caption Wanafunzi wakikusanyika mjini Pretoria

Wanafunzi weusi wanasema kuwa wamelazimishwa kuzilainisha nywele zaa wakisema kuwa hizo ni sera za kibaguzi.

Wanafunzi hao waliokuwa wamekusanyika waliimba nyimbo za zilizoimbwa wakati wa kupinga ubaguzi wa rangi na kutaka kumalizwa kwa ubaguzi.