Maafisa wa Olimpiki waachiliwa kwa dhamana Kenya

Image caption Francis Paul na Pius Ochieng waliachiliwa kwa dhamana ya dola 2000.

Mahakama nchini kenya imewaachilia wa dhamana maafisa wawili wa kamati ya kitaifa Olimpiki wanaochunguzwa kwa usimamizi mbaya wa kikosi cha kenya kilichoshiriki mashindano ya olimpiki mjini Rio.

Katibu mkuu wa kamati ya kitaifa ya olimpuni nchini Kenya (Nock) Francis Paul na Pius Ochieng ambaye ni naibu mwenyekiti wa Nock waliachiliwa kwa dhamana ya dola 2000.

Hata hivyo jaji aliwaamrisha wasiende ofisi zao, kutozungumza na mashahidi na kuwaamrisha kusalimisha paspoti zao.

Wakuu wa mashtaka walikuwa wametaka wawili hao kuzuiwa rumande kwa siku 21 wakati wanapowachunguza kwa mashtaka ya wizi, matumizi mabaya ya ofisi zao na kutelekeza majukumu yao.

Afisa mwingine Stephen Soi alikuwa tayari ameachiliwa kwa dhamana kwa misingi ya kiafya na hivyo hakuwepo mahakani.