EU: Uchaguzi wa Gabon ulikosa uwazi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa siku ya Jumane

Waangalizi kutoka muungano wa ulaya waliokuwa wakifuatilia uchaguzi mkuu nchini Gabon wanasema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa uwazi.

Rais wa sasa Ali Bongo na mshindani wake mkuu Jean Ping wote wamedai kushinda.

Bwana Ping amemtaka Bongo kukubali kushindwa na kutoa wito kwa watu wa Gabon kulinda chaguo lao.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa siku ya Jumane. Bwana Ping ambaye ni mkuu wa zamani wa muungano wa Afrika anajaribu kuung'oa utawala wa Rais Bongo ambao umekuwa madarakani kwa karibu miaka 50.