Maelfu ya watu waokolewa pwani ya Libya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Baadhi yao walipiga mbizi kuelekea kwa meli za uokoaji

Meli za wanamaji wa Uhispania na Italia zimewaokoa maelfu ya watu nje ya pwani ya Libya hii leo.

Takriban watu 3000 waliokolewa mapema leo kutoka zaii ya mashua 20 za mbao.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Baadhi yao kama huyu walisalia ndani ya mashua kuwaangalia watoto wao

Licha ya watu wengi kushangilia wakati meli za uokoaji zilipowasili na kuruka kupiga mbizi kuelekea kwa meli hizo, wengine walisalia kuwangalia watoto wao.

Shirika la habari la AP linasema kuwa idadi kubwa ya watu hao ni kutoa nchini Eritrea.