Maafisa wa Chadema wakamatwa Tanzania

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mgombea wa zamani Edward Lowassa ni kati ya waliokamatwa

Polisi nchini Tanzania wamewakamata maafisa wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema akiwemo mgombea wa zamani wa uraiswa chama hicho Edward Lowassa.

Haijulikani ni sababu ipi ilisababisha maaafisa hao kukamatwa.

Chadema kinapanga kufanya mikutano ya nchi nzima siku ya Alhamisi kupinga kile inachotaka kuwa kuingiliwa kwa haki ya kujieleka na demokrasia nchini Tanzania tangu raia John Magufuli kuingia madarakani mwaka uliopita.

Serikali ya magufuli imepiga marufuku mikutanoa ya kisiasa nchini Tanzania.