UN: Viongozi wa Sudan Kusini wawajibike

Haki miliki ya picha Filippo Grand/twitter
Image caption Filippo Gand amesema: " Viongozi wa taifa lile changa wanapaswa kuwajibika.

Afisa wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la huuma kwa wakimbizi, Filippo Grandi, amewatolea wito viongozi wa Sudan Kusini kumaliza mateso ya watu wao.

Bw Grandi alikua akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na wakimbizi Kutoka Sudan Kusini wanaoishi kambini magharibi mwa Uganda.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanakadiria kuwa zaidi ya watu 80,000 wamewasili nchini Uganda tangu kuibuka kwa mapigano ya hivi karibuni nchini humo.

Alisema: " Viongozi wa taifa lile changa wanapaswa kuwajibika."

Vikosi vya wanajeshi watiifu wa viongozi wanaohasimiana kisiasa walikabiliana kisiasa katika mji mkuu, Juba, mwezi uliopita, suala linalozorotesha mchakato wa amani uliolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.