Mapacha waliozaliwa wameungana wanajiandaa kuanza shule

Rosie na Ruby Formosa Haki miliki ya picha PA
Image caption Rosie (kushoto ) na Ruby Formosa walihitaji upasuaji wa dharura wa kuwatenganisha mwaka 2012

Mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana na kupewa uwezekano wa kuishi wa 20% wanajiandaa kuanza shule.

Rosie na Ruby Formosa walikuwa wameungana kwenye sehemu yao ya tumbo na walitumia sehemu moja ya utumbo waliyotumia kabla ya kufanyiwa upasuaji wa dharura wa kuwatenganisha mnamo mwaka 2012.

Mama yao , Angela Formosa, amesema watoto hao ambao kwa sasa wana umri wa miaka minne , kutoka eneo la la Bexleyheath Kusini mashariki mwa mji wa London ,"wanafuraha sana " ya kuanza shule.

"Miaka mmine iliyopita akilini mwangu sikufikiria kitu kama hiki kingelitokea ," alisema.

"Nilipokuwa mjamzito sikudhani nitaiona siku ya ya kwanza shuleni kwa hivyo inanifurahisha sana kwa hiyo nashukuru sana hospitari ya I Gosh [Great Ormond Street Hospital] kwa kweli."

Bi Formosa alisema ilikuwa ni taarifa ya ''kuvunja moyo'' kwake na kwa mumewe Daniel Formosa walipogundua kuwa watoto wao wa kike walikuwa na hali ya nadra ya kimatibabu, ambayo hutokea mara moja kati ya watoto 200,000 hai wanaozaliwa .

Watoto hawa wa kike walizaliwa katika hospitali ya Uversity College of London kwa upasuaji mwaka 2012 wakati mama yao Bi Formosa akiwa na ujauzito wa wiki 34.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Watoto hawa wa kike walizaliwa wakitumia sehemu ya utumbo pamoja

Baada ya saa kadhaa baada ya kuzaliwa walipelekwa katika hospitali ya Great Ormond Street Hospital kwa ajili ya upasuaji wa dharura kutokana na kuziba kwa utumbo.

Bi Formosa, mwenye umri wa miaka 35, anasema alihisi ni kama " miaka milioni "iliyopita kuwasubiri watoto hao kutoka kwenye chumba cha upasuaji .

" Muda umekwenda, siwezi kuamini jinsi muda ulivyokwenda haraka ," alisema.

" Wanafanana sana, wanaakili sana na bidii , ambayonaifahamu walikua nayo ndani ya tumbo yangu kwa sababu waliendelea kukua na kujitahidi kuishi .

Haki miliki ya picha PA
Image caption Rosie na Ruby Formosa wakisherehekea mwaka wao wa kwanza wa kuzaliwa
Haki miliki ya picha PA
Image caption Wakiwa na umri wa miaka minne wataanza shule mwezi Septemba

Profesa Paolo De Coppi, mtaalamu wa upasuaji wa watoto katika hospitali ya Gosh, amesema : "Tunafurahi kwamba Rosie na Ruby wanaanza shule Septemba mwaka huu.

" Ni furaha wakati wote kushuhudia maendeleo ya wagonjwa na kusikia kwamba wamepiga hatua kimaisha - hii inafanya kazi tunayoifanya kuwa ya kuridhisha."