Uganda na Kenya zapendwa na wataalam Afrika

Uganda ndilo taifa linalopendwa sana na wataalam Afrika
Image caption Uganda ndilo taifa linalopendwa sana na wataalam Afrika

Orodha ya maeneo mazuri na mabaya ya kuishi kwa wataalam imetolewa, na Uganda imeorodheshwa kama taifa linalopendelewa sana barani Afrika.

Taifa hilo limeorodheshwa nambari 25 duniani ,kulingana na utafiti uliochapshwa na Expat Insider.

Orodha hiyo ni kulingana na

  • Eneo lililo rahisi kuishi.
  • Kujifunza lugha inayotumiwa na wakaazi.
  • Na maisha ya kifamilia.

Kenya imeorodheshwa ya Pili Barani Afrika na ya 46 duniani.

Taifa la Nigeria limeorodheshwa la mwisho kutokana na hali ya maisha na gharama ya kuishi lakini limeonekana kuimarika ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Mada zinazohusiana