Mfungwa aapishwa kuwa Meya wa karachi

Mfungwa mmoja ameapishwa kuwa meya mpya wa mji mkuu wa Pakistan-Karachi.
Image caption Mfungwa mmoja ameapishwa kuwa meya mpya wa mji mkuu wa Pakistan-Karachi.

Mfungwa mmoja ameapishwa kuwa meya mpya wa mji mkuu wa Pakistan-Karachi.

Waseem Akhtar, kutoka ndani ya chama kimoja kikuu cha kisiasa cha MQM, alipata ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika juma lililopita.

Baada ya mahakama kufutilia mbali maombi ya kisheria dhidi yake, alitolewa gerezani hadi bustani ya mji huo mkuu na kula kiapo cha uongozi.

Waseem Akhtar alikamatwa mwezi Julai kwa kushukiwa kuwa aliwapa hifadhi magaidi pale alipokuwa waziri wa jimbo hilo miaka tisa iliyopita.

Bwana Akhtar, amesema kwamba ushindi wake ni wa kihistoria, huku akitaja mashtaka dhidi yake kuwa ni ya uwongo.