Utafiti wabaini Wasichana wa Uingereza hawana raha

Wasichana Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Watafiti waliambiwa kuwa wasichana hao wanahisi kuwa na sura mbaya na wasio na thamani.

Vijana wa kike nchi Uingereza wamekuwa watu wasio na furaha, imeelezea ripoti ya mwaka kuhusu masuala ya jamii.

Ripoti hiyo inasema kuwa vijana wa kike 10 miongoni mwa wale umri wa miaka 15, asilimia kati yao 14% hawana furaha na maisha yao kwa ujumla, na asilimia 34% wakiwa hawapendi maumbile yao.

Watafiti waliambiwa kuwa wasichana hao wanahisi kuwa na sura mbaya na wasio na thamani.

Takwimu hizo kwa England, Wales na Uskochi za katika ya mwaka 2013 na 14 zinaonyesha ongezeko kubwa la idadi ya wasichana wadogo wasio na furaha kuliko ilivyokuwa miaka mitano iliyopita.

Tofauti na wasichana, utafiti ulibaini kuwa hali ya vijana ya kuwa na furaha imeendelea kuimarika.

Watafiti wa shirika la kijamii la masuala ya watoto na chuo kikuu cha York walichunguza maisha ya watoto wa umri wa miaka 10 hadi 15

Walibaini kuwa kati ya mwaka 2009-10 na 2013-14 kwa wastani wa asilimia 11% ya wasichana na wavulana hawakuwa na furaha.

Lakini takwimu za hivi karibuni za mwaka 2013-14, zinaonyesha kuwa kiwango cha wasichana wanaosema kuwa hawana rahakimepanda kwa asilimia 14%.

Lucy Capron kutoka shirika la watoto la kijamii ameiambia BBC : "hiki si kitu ambacho kinaweza kuelezewa kwa njia ya vichocheo vya mwili (hormornes) au kwa sababu tu asilia za ukuaji, kwa kweli hiki ni kitu tunachohitaji kukiangalia kwa makini na kinachohitaji kushughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi."

Idadi ya vijana wa kike walioripoti kuwa na wasi wasi wa sura na maumbile yao iliongezeka kwa asilimia 30% kwa kipindi chote hadi asilimia 34% katika mwaka 2013-14 - huku idadi ya wavulana ambao hawana raha kuhusu sura na maumbile yao haikubadilika kwani ilisalia kuwa asilimia 20%.