Ali Bongo: Komeni kuingilia maswala ya Gabon

Rais Ali Bongo wa Gabon Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Ali Bongo wa Gabon

Msemaji wa rais wa Gabon Ali Bongo ambaye anataka kuendelea kusalia mamlakani ameyataka mataifa ya kigeni kutoingilia maswala ya taifa hilo.

Amekishtumu chama cha kisosholisti cha rais Francois Hollande kwa kuegemea upande wa kiongozi wa upinzani Jean Ping mbali na kutaka kuingilia shughuli ya uchaguzi nchini Gabon.

Chama cha bwana Hollande kilitoa taarifa siku mbili zilizopita kikisema mabadiliko ya uongozi yatakuwa ishara na mfano mzuri.

Tayari rais wa Ivory Coast Allasane Outtara amemfuta kazi mshauri wake aneyetuhumiwa kuingilia shughuli za uchaguzi wa Gabon.

Tume ya uchaguzi nchini Gabon hatimaye imekutana mapema siku ya Jumatano ili kuanza kujumlisha matokeo kutoka maeneo tofauti ya taifa hilo.

Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika hapo jana jioni.

Matokeo rasmi yatachelewa kwa siku moja.

Mada zinazohusiana