Upinzani wataka kura kuhesabiwa upya Gabon

Kiongozi wa upinzani nchini Gabon Jean Ping
Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Gabon Jean Ping

Huku wapiga kura wakisubiri matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo,chama cha upinzani kimetaka kura kuhesabiwa tena ,kufuatia ripoti zisizo rasmi ambazo zinampa ushindi rais Ali Bongo kulingana na chombo cha habari cha reuters.

Kambi ya Jean Ping imepinga idadi ya asilimia 99.9 illiojitokeza kupiga kura katika mkoa wa Haut Ogooue,Reuters imeongezea ikimnukuu msemaji.

Haut Ogooue ni ngome ya kabila la Teke la rais Bongo kulingana na chombo cha habari cha AFP.

Waangalizi wa muungano wa Ulaya wameitaka Gabon kuchapisha maelezo ya matokeo katika kila kituo huku ukitoa wito kwa washiriki kuweka amani.