Usajili uliofanyika siku ya mwisho barani ulaya

David Luis Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Luis arejea Chelsea

Vilabu vya soka barani ulaya vimefanya usajili wa kuimarisha vikosi vyao katika siku ya mwisho ya usajili uliofungwa usiku wa kuamkia Septemba moja.

Chelsea wamemrejesha beki wao kisiki David Luiz toka Paris St- Germain, mchezaji huyu kanunuliwa kwa kiasi cha pauni million 34. Pia Chelsea imemsajili Marcos Alonso toka Fiorentina kwa pauni milion 23.

Moussa Sissoko amesaliwa na Tottenham akitokea Newcastle kwa pauni milioni 30, Leicester City wamesajili Islam Slimani toka Sporting Lisbon kwa pauni 29.

Stoke City wamemsajili Wilfried Bony kwa mkopo toka Manchester City, Samir Nasri nae amepelekwa kwa mkopo Sevilla toka kwa matajiri wa Man City

Mshambuliaji Mario Balotelli wa Liverpool amesajili na Nice ya ufaransa bure, West Ham wamsajili beki Alvaro Arbeloa toka Real Madrid,

Valencia ya Hispania wamesamjili kwa mkopo wa muda mrefu Eliaquim Mangala wa Manchester City, Nao Juventus wamemsajili Juan Cuadrado kwa mkopo toka Chelsea kwa mkataba wa miaka mitatu.

Jack Wilshere ametua Bournemouth kwa mkopo wa msimu mzima, Mshambuliaji Mkongo Dieumerci Mbokani asajiliwa na Hull City. Enner Valencia aenda Everton kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka West Ham.