Schweinsteiger ,Keane wastaafu soka la kimataifa

Bastian Schweinsteiger Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bastian Schweinsteiger

Mshambuliaji Robbie Keane wa Jamuhuri ya Ireland na kiungo wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger wamestaafu kuzichezea timu zao za taifa.

Schweinsteiger aliagwa na wachezaji wenzake baada ya kumalizika mchezo kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Finland, ambapo Ujeruman walishinda kwa ushindi wa mabao 2-0.

Kiungo huyu alianza kukichezea kikosi cha wakubwa cha timu ya taifa mwaka 2004 na kucheza jumla ya michezo 121 huku akiwa kafunga mabao 24

Nae mshambuliaji wa Jamuhuri ya Ireland Robbie Keane aliachana na soka la kimataifa baada ya mchezo wa timu yake na timu ya taifa ya Oman,Keane alifunga bao moja katika mchezo huu walioibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mshambuliaji huyu ameichezea timu ya taifa michezo 146 na kufunga mabao 68.