Uingereza: 18% ya wazazi wanajutia majina ya watoto wao

Mtoto mchanga Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mama mmoja alisema: "mwanangu huchukia jina lake, na hunifanya nijihisi vibaya kwa kulichagua."

Baadhi ya wazazi nchini Uingereza wanasema wanajutia majina waliyowachaguliwa watoto wao, umebaini utafiti.

Utafiti huo uliofanywa kupitia kura ya maoni iliyowahusisha wazazi zaidi ya 1,000 uliyofanywa na shirika la Mumsnet, ulibaini kuwa 18% ya wazazi walijutia majina waliyoyachagua kwa vizazi vyao, lakini ni 2% kati yao walioamua kubadilisha majina ya watoto wao.

Sababu kuu ya kujutia ilikuwa ni jinsi majina yanavyotumiwa mara kwa mara na watu wengine ambapo 25% ya taarifa zilibaini.

Sababu nyingine za kujutia majina hayo zilikuwa ni herufi zake na suala la namna yanavyotamkwa. Suala hilo lilikuwa kwa kiwango cha 11%.

Utafiti wa Mumsnet umetolewa sambamba na takwimu za mwaka kutoka ofisi ya kitaifa ya takwimu kuhusu majina yaliyo maarufu zaidi ya watoto ya mwaka katika maeneo ya England na Wales.

Justine Roberts, muasisi wa shirika la wazazi Mumsnet, anasema : "kutafuta jina la mtoto wako ni moja ya mambo ya kwanza anayoyafanya mzazi, kwa hiyo kwa kwa njia fulani kujutia jina ulilompa mtoto ni sehemu ya uzazi -unafanya kazi ngumu na kufanya utafiti, kujaribu kuwafurahisha watu kadhaa kwa wakati mmoja , na unaishia kufanya makosa.

"La kuliwaza ni kwamba wengi wa watoto hukua wakitumia majina hayo, na wale ambao hawawezi, wanaweza wakati wowote kutumia majina yao ya kati, na majina ya bandia ."

Kwa mujibu wa utafiti huo mama mmoja alisema alianza kujutia jina alilomuita mwanae Elsa wakati Filamu ya Disney Frozen ilipokuwa maarufu.

Mama mwingine alisema: "mwanangu huchukia jina lake, na hunifanya nijihisi vibaya kwa kulichagua."

Huku mzazi mwingine akisema jina la mwanae "lilichukuliwa na kundi la kikaidi,mara baada ya kuzaliwa".

Mwaka jana Oliver na Amelia yalitangazwa kuwa ndio majina yaliyo maarufu zaidi katika England na Wales, huku Emily na Jack yakiongoza kwa umaarufu Uskochi.