Yeyote mwenye HIV kupata tiba Afrika Kusini kuanzia leo

Mwanaharakati akionyesha bango la tiba kwa wote Haki miliki ya picha AFP
Image caption Utafiti wa Shirika la afya duniani (WHO) ulibaini kuwa kuwatibu watu wote wanaoishi na HIV mapema iwezekanavyo husaidia kuboresha afya na kurefusha zaidi maisha

Kuanzia leo yeyote nchini Afrika kusini mwenye virusi vya HIV atapata tiba ya madawa ya kupunguza makali (ARV) kutoka kwa serikali kabla ya kuugua ukimwi.

Hii ni habari njema kwa watu zaidi ya milioni nne wanaoishi na virusi hivyo, lakini bado hawajapata matibabu.

Utafiti wa Shirika la afya duniani (WHO) ulibaini kuwa kuwatibu watu wote wanaoishi na HIV mapema iwezekanavyo husaidia kuboresha afya na kurefusha zaidi maisha yao.

Hadi kuchukuliwa kwa hatua hii mpya kwa watu wanaoishi na virusi vay HIV wenye kiwango cha CD4- kipimo kinachotumiwa kupima udhabiti wa mfumo wa kinga ya mwili - chini ya 500 tu walikua ndio waliokuwa wakipewa matibabu kutoka kwa serikali, ameiambia BBC msemaji waziri wa afya Joe.

''Hii itaongeza kiwango cha wastani wa kuishi walau kufikia umei wa miaka kufikia 2030." Amesema.

Kwa sasa makadirio ya umri wa kuishi nchini Afrika kusini ni miaka 63.

Afrika Kusini ina mpango mkubwa zaidi wa tiba ya virusi vya HIV duniani na ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu wanaoishi na virusi vya hivyo vinavyosababisha ukimwi duniani.