Seneta afananishwa na 'kahaba mwenye hasira' Australia

Seneta Jacqui Lambie
Maelezo ya picha,

Seneta Jacqui Lambie

Seneta mmoja anayependa kuzungumza sana nchini Australia amemfananisha na ''kahaba mwenye hasira'' mwenzake wa chama cha kihafidhina kabla ya kuomba msamaha kwa makahaba.

Seneta huyo Jacqui Lambie ana historia ya kuzozana na seneta wa serikali Cory Bernadi.

Bernadi wiki hii alimkosoa Seneta wa chama cha Leba sam Dastyari ambaye ghrama yake ya kusafiri ililipwa na mfadhili mmoja wa Uchina.

Seneta Lambia alimfananisha bwana Bernadi na kahaba ambaye alikuwa anatoa ushauri kuhusu ujane.

''Kabla ya sijashtumiwa na makahaba ,ninaomba msamaha kwa kuwafananisha na Seneta Bernadi .