Uzbekistan waomboleza kifo cha rais Islam Karimov

Islam Karimov inadaiwa kaaga dunia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Islam Karimov

Watangazaji waandamizi wa runinga ya taifa na viongozi wakuu wa serikali nchini Uzbekistan wametuma ujumbe wa tanzia katika mitandao ya kijamii kufuatia kuzagaa kwa uvumi kuwa rais Islam Karimov ameaga dunia.

Wafanyakazi wa umma katika mji wa Samarkand alikozaliwa rais huyo,wamejikusanya na kufanya usafi katika mitaa mbalimbali kama sehemu ya maandalizi ya mazishi na maziko ya rais huyo ingawa haijathibitika mara moja.

Karimov ameliongoza taifa hilo la Uzbekistan kwa zaidi ya robo ya karne sasa.mapema wiki hii, mmoja kati ya watoto wake aliarifu kuwa babake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ubongo wake kuvia damu, ingawa serikali haijatoa tamko lolote kuhusiana na hali ya kiongozi huyo.