Muitaliano Fabio Borini aumia misuli ya paja

aumia nyama za paja Haki miliki ya picha Google
Image caption Fabio Borini

Mshambuliaji wa klabu ya Sunderland Muitaliano Fabio Borini atakua nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu sababu ya maumivu ya nyama za paja.Borini aliumia misuli ya paja wakati akipiga mpira wa adhabu ya kutenga katika mchezo wa mwisho wa wili iliyopita dhidi ya Southampton.

Kuumia kwa mchezaji huyu kunaifanya timu ya Sunderland kubakiwa na mshambuliaji mmoja wa kiwango cha juu ambae ni Jermain Defoe,pamoja na kinda Joel Asoro mwenye miaka 17.

Sunderland ama Paka weusi walishinda kukamilisha usajili wa mshambuliaji Steven Naismith, toka Norwich kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba mosi.

Hivyo meneja wa timu hiyo David Moyes anakibarua cha kuwabadilishia majukumu mawinga Duncan Watmore na Adnan Januzaj,kuwa washambuliaji wa kati.